Sugu na Mkewe Wapata Mtoto wa Kiume

Aliyekuwa msanii wa muziki wa hip hop Bongo na sasa Mbunge wa Mbeya Mjini (CHADEMA), Joseph Mbilinyi 'Sugu', yeye na mkewe wamejaliwa kupata mtoto wa kiume.

Mbunge huyo ameeleza kuwa mkewe na mtoto hadi sasa wanaendelea vizuri. Kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram ameandika;

"Tunamshukuru sana Mungu, usiku wa kuamkia leo tarehe 15 Mei 2019 ametujalia mtoto wa kiume. Mama na mtoto wote wanaendelea vizuri," ameeeleza.

Ameendelea kwa kusema, "Asanteni sana wote hasa kwa maombi na kututakia mema kwenye kipindi chote cha ujauzito wa Happiness. Hakika nina furaha isiyo kifani,".


HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA UDAKU SPECIAL >BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIALLoading...

Sugu na Mkewe Wapata Mtoto wa Kiume Sugu na Mkewe Wapata Mtoto wa Kiume Reviewed by Udaku Special on May 15, 2019 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.