Ubosi Unanifanya Nisiolewe, Umri Unazidi Kusonga..Naombeni UshauriTangu nimalize harakati za masomo ni miaka 6 sasa. Wenzangu wote niliyokuwa nao ama wameolewa na kupata watoto ama wamepata watoto nje ya ndoa.

Mimi tangu nikiwa mdogo na kwa maadili niliyolelewa niliapa kutokuzaa nje ya ndoa. Lakini mpaka sasa nina miaka 33 sijapata mume wa kunioa.

Mbaya zaidi kwa sasa nina cheo kazini kwangu, basi kila mwanaume ananiogopa. Hapa nauona uzee unasogea sina mume wala mtoto.

Najiuliza, nivunje kiapo changu cha kutokuzaa nje ya ndoa ama niendelee kusubiria mume nisiyejua atapatikana lini na huku umri unaenda?

Niko njia panda jamani naombeni ushauri.

đŸ’¥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SERIKALINI

đŸ’¥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SEKTA BINAFSI

đŸ’¥NAFASI ZA INTERSHIP MAKAMPUNI MBALI MBALI

Tags

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
 1. fANYA MAAMUZI MAGUMU UACHE KUA NJIA PANDA.KWANI KIAPO CHAKO NI CHAMAISHA?
  THINGS DO CHANGE IN ACCORDANCE TO TIME AND NATURE.FIRST OF ALL JITATHIMINI UJUE NI KWANINI HUPATI MUME?(NI CHEO ULICHONACHO KWA SASA?HOW ABOUT BEFORE HUJAPATA CHEO?UNACHAGUA SANA WANAUME?YOU WANT UR CLASS LEVEL?MAYBE UR CHARACTER?AU UNA KASORO YOYOTE KATIKA MAUMBILE YAKO?HOW ABOUT RELIGION?).THEN MAKE A DECISION

  ReplyDelete
  Replies
  1. Mtoto nje ya ndoa unatafuta shida za baadaye na kumharibia mtoto huyop maisha yake yote atakuwa bila baba figure. Usisubiri mwanaume akutafute tafuta wewe mwenyewe mwanaume atakaye kufaa wote watakao kufuata wanataka kupanda daladala kisha watateremka kituo cha mbele. Blessings and trust God and follow his purpose in your life.

   Delete
 2. naomba tuonane tuongee
  nina shida inayo oana n yako huwenda ikatupa jibu fulani

  ReplyDelete
 3. mimi sioni kama umri wako umeenda kivile sema sauti ya shetani inapiga kelele zaidi masikioni mwako,ila ninachofahamu Mungu ana mpango mzuri na wewe kama utaamua kumuelekea kwa moyo wako wote,tatizo watu wengi wanataka vya Mungu hawamtaki Mungu.....kipo kinachozuia kukijua ni Mungu akufunulie siri.Kama ujampa Yesu maisha yako mpe...kama tayari tafuta kujua siri kwa kumtumia Roho Mtakatifu.

  ReplyDelete
 4. Make choice of loose or gain
  Ur personality can be the big factor.
  Nikwel umri umeenda lakini unaihitaji mtoto ama mme ..maan unaweza kuolewa lakini ukakosa mtoto vilevile ...so Kila kiu kina sababu yake

  ReplyDelete
 5. This comment has been removed by the author.

  ReplyDelete
 6. Kila Jambo Lina wakati wake Nina imani mpaka unafikia kuwaza hilo swala Sasa muda umefika mshirikishe Mungu bado hujachelewa ni muda mwafaka.

  ReplyDelete
 7. Asalaam naomba tuwasiliane kuptia namba hii rafiki 0788 673152

  ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad