6/18/2019

Breaking News: Rais Magufuli Atengua na Kuteua


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli, ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala ya Nishati ya Umeme Vijijini (REA), Michael Pius Nyagoga.

Taarifa ya Ikulu iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais,  Ikulu Gerson Msigwa, utenguzi huo umeanza leo Juni 17, 2019.

Aidha kutokana na uamuzi huo, Rais Magufuli amemteua Wakili Julius B. Kalolo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala ya Nishati ya Umeme Vijijini (REA), kuanzia leo Juni 17, 2019.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

1 comment:

  1. Uteuzi huu mpya wa Mwenyekiti wa Bodi hii unaweza ukawa ni chachu ya utekelezaji wa usambazaji umeme hasa vijijini katika Wilaya ya Misenyi, Mkoani Kagera ambapo kwa miaka mitatu ikidaiwa kwamba nguzo na waya ikidaiwa ni changamoto kupatikana kwake! Kata ya Buyango ni zaidi hasa kijiji Rutunga!

    ReplyDelete

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger