Ex wa Diddy azua mapya, adai alilipwa pesa kutoa ujauzito

Baada ya rappa P Diddy kuanzisha mahusiano mapya na mwanadada Gina Huyn miezi kadhaa iliyopita na baadae kuripotiwa kuwa wawili hao wameachana sasa kupitia mahojiano ya kipindi cha “Unwine with Tasha K” Gina amefunga vitu kibao kumuhusu Diddy.

Gina Huyn amefunguka na kuweka wazi kuwa Diddy alikuwa akimnyanyasa kwa kumpiga na ilifikiwa hatua alipokuwa mjamzito alilazimishwa kufanya utoaji wa mimba na kulipwa kiasi cha dola za Kimarekani 50,000 sawa na zaidi ya shilingi Mil.100 za Kitanzania, Gina alienda mbali na kusema amekuwa na Diddy kwenye mahusiano yenye manyanyaso kwa miaka mitano tokea mwaka 2014-2019.“Mara ya kwanza nilipata ujauzito na Diddy ilikua ni Oktoba 2014 nilimuambia kuhusu ujauzito na aliniambia kuwa nitoe na alinipa kiasi cha zaidi ya shilingi mil.100 ili niishughulikie mimba ile lakini nilimpenda kweli na sikutaka kumuonyesha kuwa sikuwepo pale kwa ajili ya pesa zake na nilitaka awe mtu mzuri kwangu”

“Mara ya kwanza alikua mtu mzuri sana kwangu lakini ndani ya miaka mitatu alibadilika alianza kuwa na vurugu kihisia, kifikra mara nyingi alikua akinilinganisha na Cassie na kusema kuwa mimi sio mtu mzuri kama Cassie” >>> alisema Gina That Gal ya Rosa Ree Yawa Gumzo Itazame Hapa chini:

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments