Mauaji ya Mwanafunzi wa Chuo cha Kampala, Mambosasa Aapa Kuwajibu Wauaji kwa Muda Mfupi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar Es Salaam ametoa pole kwa niaba ya jeshi la Polisi kwa ndugu  kwa kuondokewa na Mwanafamilia Anifa Mgaya ambaye ni Mwanafunzi wa Chuo cha Kampala.

"Kwa niaba ya Jeshi la Polisi tunatoa pole kwa Ndugu yetu Chacha kwa kuondokewa na Mwanafamilia katika kifo hiki ambacho hakijatarajiwa, ni cha ghafla na tumekipokea kwa masikitiko sana, hivyo tukuhakikishie tutaendelea kuwa pamoja nawe na msiba huu wa ghafla hauwezi kwenda hivihivi," Kamanda Mambosasa.

Aidha Kamanda Mambosasa amesema kuwa wahalifu hao watajibiwa kwa muda mfupi kwa kitendo walichokifanya kuondoa uhai wa mwanafunzi huyo.

Kamanda Mambosasa ameyasema hayo wakati wa kuuaga mwili wa marehemu Anifa Mgaya aliyekuwa Mwanafunzi wa Chuo cha Kampala Dar es salaam aliyeuawa juzi ikiaminika kuchomwa kisu na Wezi, Marehemu alizaliwa Februari 09, 1997.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad