Rooney Amchana Kocha wa Man United "Hata Ukiwasajili Ronaldo na Messi Awawezi Kutatua Tatizo la Timu"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Usajili wa nyota wa soka duniani akiwemo Lionel Messi, Cristiano Ronaldo, Gareth Bale na Sergio Ramos hauweza kutatua matatizo katika klabu ya Man United, kulingana na nahodha wake wa zamani Wayne Rooney. Rooney, ambaye anaichezea klabu ya DC United nchini Marekani , hadhani kwamba kikosi cha Ole Gunnar Solskjaer kitaweza kushindana na timu nyengine msimu ujao.



”Kitu cha kwanza ambacho Ole anafaa kufanya ni kujenga kikosi hicho na sidhani kuleta mchezaji mwenye thamani £100m kutawasaidia wachezaji waliopo” , alisema nahodha huyo wa zamani wa timu ya Uingereza, 33.

Akizungumza na BBC aliongezea, ”,Ole angenunua wachezaji walio na thamani ya kati ya £30-40m wenye uwezo na baadaye kukijenga kikosi chake kutokana na wachezaji watano ama sita.

Unaweza kuwaleta wachezaji kama Messi, na mshambuliaji wa Juventus Ronaldo , Ramos na Bale lakini itakugharimu £350m na baada ya miaka miwili fedha hizo zimepotea.

Mshambuilaji wa Barcelona Lionel Messi na yule wa Juventus Ronaldo wameshinda mataji 10 ya balon D’Or huku nahodha wa Real Madrid Ramos, 33, akiwa ameshinda kombe la dunia, ubingwa wa Ulaya na mataji manne ya ligi ya mbaingwa.

Mchezaji mwenza wa Ramos, Bale, 29, ameshinda taji hilo la Ulaya mara nne na kwa kipindi kirefu amehusishwa na uhamisho wa kuelekea Old Trafford.

Rooney anataraji kwamba utakuwa wakati mgumu wa Solskjaer ambaye amehusishwa na uhamisho wa wachezaji kadhaa , ikiwemo beki wa Ajax Matthijs de Ligt.

Solskjaer, ambaye alimrithi Jose Mourinho kama mkufunzi wa United ameanza kujenga kikosi chake huku winga wa Swansea Daniel James 21 akiwa wa kwanza kuelekea Old Trafford.

Rooney ambaye amewahi kuwa mfungaji wa magoli mengi akiichezea United na Uingereza alisema: Klabu inafaa kujengwa na wachezaji wachanga lakini ni sharti wawe wazuri wa haja na nafikiri mashabiki wataelewa kwamba huenda wasipiganie taji la ligi mwaka ujao.

Wacha Ole awe na kikosi atakachokijenga kwa kipindi cha miaka miwili au mitatu ambacho kitaweza kupigania ligi ya Uingereza na ile ya mabingwa Ulaya.

Ni timu kama vile Chelsea, Arsenal na Tottenham na hususan Everton ambazo zitahitaji kipindi cha miaka miwili kufikia kiwango cha Liverpool na Manchester City.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad