6/10/2019

Serikali Kutibu Bure Watoto Watakaougua Ugonjwa wa Selimundo

Serikali imesema imeandaa mpango wa kutoa matibabu ya bure kwa watoto watakaokuwa wakiugua ugonjwa wa Selimundu, kwa kupatiwa vibali maalum vya huduma bila malipo kufuatia kufanyiwa uhakiki kwa familia zisizojiweza.


Kauli hiyo imetolewa Bungeni na Naibu Waziri wa Afya Maendeleo Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Dr Faustine Ndugulile, wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Taska Mbogo, ambaye alihoji juu ya wagonjwa hao kupewa matibabu ya bure.

Mbunge amehoji kuwa "Serikali ina mpango gani kuwasaidia wagonjwa wa Sickle cell (Seli mundu) ili watibiwe bure?"

Akijibu swali  Naibu Waziri wa Afya Dr. Faustine Ndugulile amesema kuwa "kupitia Wizara ya Afya tumeandaa muongozo wa kutoa msamaha kwa wagonjwa wa Sickle cell (Seli mundu), familia zisizojiweza zitahakikiwa na kupewa kibali cha huduma bila malipo. Serikali inaanzisha mpango wa taifa kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza."

Kwa sasa Bunge linandelea jijini Dodoma ambapo Mawaziri mbalimbali wameendelea kuwasilisha Makadirio yao ya Bajeti kwenye Wizara zao.HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger