Siku 7 za Wema Sepetu gerezani zamtesa Aunt Ezekiel

advertise here
Ni siku mbili zimepita tokea Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuamuru muigizaji Wema Sepetu kupelekwa gerezani siku saba ambapo amri hiyo ilikuja June 17,2019 huku sababu ikitajwa kuwa alikiuka masharti ya dhamana.

Muigizaji mwenzake ambaye pia ni rafiki wa karibu na Wema Sepetu, Aunt Ezekiel ameonekana kuguswa na amri hiyo iliyotolewa na Mahakama na kumkumbuka rafiki yake ambapo ametumia ukurasa wake wa instagram kupost picha nyingi za Wema na kuandika maneno ya matumaini kwamba ipo siku yote haya yatapita na Wema atabaki kuwa rafiki mzuri kwake.“Ni vizuri pale watu wasiojuana kuwa marafiki lakini ni huzuni pale marafiki wawili wanapokuwa hawajuani tena ,Utabaki kuwa Rafiki Mzuri kwangu daima ,Inshallah hili Pia litapita šŸ˜¢šŸ™” >>>aliandika Aunt Ezekiel

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE