6/11/2019

Simba yashindwa kujizuia, yafunguka sakata la Bocco kusaini klabu ya Afrika Kusini,

Miamba ya soka nchini Tanzania Simba SC, hatimaye imefunguka juu ya sakata linalomuhusu nyota wao John Bocco kuhusishwa na kusajiliwa na klabu nyingine kutoka Afrika Kusini.Katika taarifa yao kupitia akaunti ya kijamii ya Instagram, Simba imefafanua sintofahamu hiyo na kusema kuwa swala hilo lilishazungumzwa baina yao na klabu ya Polokwame ya Afrika Kusini na kumalizwa kwa maslahi ya pande zote mbili.

John Bocco amesaini mkataba mpya wa miaka miwili hapo juzi kuendelea kuichezea Simba. Bocco ambaye alikuwa mchezaji bora wa Simba na Ligi Kuu kwa msimu wa 2017/18 na Mshambuliaji Bora kwa msimu wa 2018/19 amefunga jumla ya mabao 30 ya Ligi katika misimu miwili.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger