Wanawake/Wasichana wa Aina Hii ni Hatari Sana Kuwa Nao Kimapenzi

 NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPADemu wako wa zamani

Ni vizuri kutorudia mahusiano ya zamani na zaidi kama kwenye mahusiano yenu ya mwanzo mambo hayakuishia kwa uzuri. Sababu kuu ya msingi, kiukweli ni kwamba hakika mwanzoni mlikuwa hamuendani na ndio sababu ya iliyopelekea kuvunjika kwa mahusiano yenu, ndani ya hizo sababu kuna vitu vilivyopolekea kutokea kwa hayo, ukichunguza na kuziangalia kwa makini utagundua ni za asili na ambazo si rahisi kwa mmoja wenu kuzibadilisha sababu ni vitu au mambo ambayo yatakuwa ni ya damuni.

Dada wa rafiki yako kipenzi

Epukana na kujiingiza kwenye mahusiano na dada wa rafiki yako. Si tu kwamba utaweza kujiingiza kwenye uhasama na chuki kama mambo hayatakwenda sawa, ila pia utaweza kujiweka kwenye mazingira ya kujikuta siku moja unapigwa hata ngumi za uso sababu tu ulimuumiza dada yake. Pia, utaweza kumkosa mtu ambaye ndie alikuwa ni kimbilio lako kwa mambo mbalimbali pale ambapo itatokea wewe na dada yake mambo kutokwenda sawa, sababu hapo patakuwa na mgongano wa kimaslahi kwa huyo rafiki yako.

Wanawake wenye mambo mengi

Kiukweli, kutoka na watu kama hawa kinaweza kuwa ni kitu cha kufurahisha, ila mwisho wa siku itakuingiza kwenye matatizo. Mara zote kumbuka ni vyema kuwa salama kuliko kujuta. Usijiingize kwenye majaribu ambayo utakuja kuyajutia kwa maisha yako yote.

Wanawake wanaopenda hela kupitiliza (Wachunaji)

Kuwa mbali nao, labda kama unataka salio lako limalizike pasipo wewe kujifahamu. Naamini hili kila mmoja analifahamu na halihitaji darasa zaidi.

Demu wa zamani wa rafiki yako

Kama unathamini urafiki wako na mshikaji wako achana na habari ya kutoka na aliyekuwa demu wake. Mambo yanaweza kubadilika na kuwa kama au zaidi ya yaliyotokea kwa rafiki yako na ikaja kula kwako zaidi. Wakati mwengine inaweza tengeneza chuki kati yako na rafiki yako, huku akiamini kwamba ulikuwa unatoka au kumnyemelea demu wake toka zamani.

STORI ZAIDI za AINA HII Download Udaku Spesho App HAPA

Wadau mademu wapo wengi sana, fanya kutafuta wengine nje ya hawa….. ni ushauri tu.

 NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPA


 JINSI YA KUANDIKA CV BORA BONYEZA HAPA 

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad