Amchoma Kisu ‘House Boy’ Kwa Kumkuta na Mkewe

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Maisha ya kibarua mmoja (house boy) katika Kaunti ya Kirinyaga nchini Kenya yako hatarini baada ya kuchomwa kisu na mwanaume ambaye alimkuta kitandani na mkewe.

Inadaiwa kuwa mume huyo alikuwa ameondoka nyumbani kuelekea kazini Jumatatu asubuhi, lakini akagundua alikuwa amesahau kitambulisho.

Hata hivyo, aliporejea nyumbani alishangaa kumkuta mfanyakazi huyo kitandani na mkewe, ndipo akapandwa na hasira na kuchukua kisu, akamdunga mikononi na sehemu nyingine za mwili, akimsababishia majeraha tele mwilini.

Mshukiwa alipiga mayowe akitafuta msaadaa, mayowe yake yaliwashtua wakazi wengi ambao walimwokoa na kumkimbiza katika hospitali ya binafsi ya White Rose, ambapo bado anatibiwa baada ya kushonwa majeraha.

Mume husika alikamatwa na polisi wa utawala eneo hilo na bado anazuiliwa akihojiwa, wakazi wakisema alikuwa karibu kumuua mfanyakazi huyo.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad