Bashiru "Mchwa wa CCM Waliokula Fedha za Chama Sasa Wanateseka Kutafuta Huruma ya watu"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk Bashiru Ally amesema baadhi ya wanachama wa hicho aliowafananishwa na mchwa hivi sasa wamebanwa na hawawezi tena kutafuna fedha wala kufuja mali za chama hicho.

Amesema wanachama hao wanapokumbushwa wajibu wao na kuachana na tabia hiyo wanageuka mbogo na kuanza kuzungumza mambo yasiyofaa kusaka huruma ya watu.

Ametoa kauli hiyo leo Jumanne Julai 23, 2019 mkoani Dodoma wakati akizungumza na wanachama wa CCM mkoani humo katika uzinduzi wa vibanda vya biashara.

Dk Bashiru amesema baada ya watu hao kubanwa na mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli wanazungumza ujinga nje ya utaratibu wa chama hicho.

Amesema miaka ya nyuma walikuwepo waliotafuna fedha na kuifanya akaunti ya CCM kwa mwaka kuwa na Sh milioni 5 wakati hivi sasa kwa mwaka akaunti inakuwa na hadi Sh bilioni 20.

Bashiru amesema watu wa aina hiyo hawatavumiliwa, watashughulikiwa na kuwataka waondoke wenyewe kuliko kuendelea kukivuruga chama,”

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Swadakta kaibu wangu.
    Tena wajitathmini na wapote kama walivyo ambiwa na Wa Mtama.
    Woote wanajijua na wangatuke wenyewe.
    Ubadhirifu umefikia Kikomo.
    Na hatuutaki tumeuchukia.
    Kidumu chama cha Mapinduzi...!!!

    ReplyDelete

Top Post Ad