Dk. Shein amtumia salamu za rambirambi Bakhresa Kufuatia Vifo vya Wafanyakazi Watano wa Azam

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, amemtumia salamu za rambirambi Mwenyekiti wa Makampuni ya Bakhresa, Said Salim Bakhressa kutokana na vifo vya wafanyakazi watano wa Azam Media Limited kutokana na ajali ya barabarani.

Ajali hiyo Jumatatu katika eneo la katikati ya Igunga (Tabora) na Shelui (Singida) ambapo wafanyakazi hao pamoja na madereva wawili waliofariki dunia baada ya basi aina ya Coaster waliokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na gari la mizigo wakati wakielekea wilayani Chato kwa ajili ya uzinduzi wa hifadhi hiyo ya Taifa ya Chato-Burigi.

Katika salamu hizo za rambirambi Rais Shein alieleza kuwa amepokea kwa mshtuko na huzuni kubwa taarifa ya ajali hio na kwamba yeye binafsi pamoja na wananchi wote wa Zanzibar na Tanzania nzima kwa jumla wamejawa na simanzi nzito kutokana na vifo vya wafanyakazi hao.

"Kutokana na msiba huu, natoa salamu za rambirambi kwako Said Salim Bakhressa, ndugu, wanafamilia wa marehemu, marafiki, wafanyakazi wote wa Makampuni ya S.S. Bakhressa pamoja na watazamaji, wasikilizaji na wafuatiliaji wa vipindi na habari mbali mbali zinazotolewa na Azam Media Limited, ndani na nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania"ilieleza sehemu ya salamu za rambirambi alizozituma Dk Shein."

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad