Irene Uwoya, Amber Lulu Wakubali Yaishe Waomba Radhi Hadharani

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Wasanii wa tasnia ya muziki wa Bongo Fleva na Bongo Movie hapa nchini, Irene Uwoya pamoja na Amber Lulu wamekubali makosa yao na wameomba radhi kwa vitu ambavyo wamevifanya mbele za watu.


Wawili hao wameomba radhi siku ya jana kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram, baada ya Irene Uwoya kumwaga pesa mbele ya wanahabari hali iliyopelekea uharibifu wa vitendea kazi mbalimbali, huku Amber Lulu akidaiwa kutumia lugha chafu kwa Hamisa Mobetto, Dj pamoja na washindani wa Miss Kinondoni siku ya Jumamosi.

“Ndugu zangu wahandishi wa habari, niliamua kutoa pesa kwa 'style' ya kutunza, nawaomba radhi sana sikuwa na nia mbaya juu yenu, sikufanya hivo kwa lengo la kuwadhalilisha kama ilivyotafsiriwa, Pia kuhusu kuwaomba kuvaa suti nilikua na maana nzuri katika utanashati wenu wa kila siku, kwa zaidi naomba radhi kwa yeyote aliyekwazika kwa namna moja au tofauti”, ameandika Uwoya.

Aidha kwa upande wa msanii Amber Lulu yeye ameandika, “naomba radhi, sisi sote ni watu wenye mapungufu, kwa kusema hivyo naamini kila mtu anaweza kukosea, naomba radhi na kwa unyenyekevu naomba samahani kwa kile kilichotokea usiku wa Miss Kinondoni, na sikua katika hali maridhawa na tengamavu natambua nilipoteleza naomba radhi kwa yeyote niliemchukiza.”
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad