Jeshi la Polisi atoa tahadhari uwepo wa pesa bandia

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mwanaume aliefahamika kwa jina la Samwel Temu (40) mkazi wa Sanawari jijini Arusha , anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Manyara kwa kosa la kukutwa na noti bandia nane za elfu kumi kitendo ambacho ni kosa la jinai.

Mtu huyo alikamatwa huko Songambele kata ya Mirerani wilaya ya Simanjiro mkoani hapa July 14 mwaka huu.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Manyara, Augustino Senga amesema pesa hizo zilikuwa na namba BX9269744-2, RT9463413-2, CS2723694, CT6427252, BX9269733, CT6427255 pamoja na pesa halali kiasi cha shilingi 21,000/= ambazo amerudishiwa chenchi baada ya kutoa noti bandia.

Aidha Kamanda Senga amewatahadharisha wananchi wa Mkoa wa Manyara kuwa makini na fedha za mtuhumiwa huyo ambazo tayari zipo kwenye mzunguko.

Jeshi la polisi limeeleza kuwa limefanya mahojiano ya kina  na mtuhumiwa huyo kujua mtandao wake ili kuweza kuwasaka washiriki wenzake na kutokomeza kabisa mtandao huo unaotengeneza pesa bandia.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad