Mama Diamond, Baba Diamond ‘Halisi’ Kumenoga

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Wazazi wa Msanii nyota wa Bongo Fleva nchini Diamond Platnumz ni kama waneonesheana umwamba kutokana na wawili hao kuonekana wakiwa katika hali za mahaba na wenza wao kwa nyakati tofauti.

Hivi karibuni baba yake Diamond kunaswa live akiwa kimahaba msituni na msanii wa muziki na filamu za Kibongo, Baby Madaha na mama wa mwanamuziki huyo, Sanura Kassim ‘Sandra’ naye amejibu mapigo.



Mama Diamond au Mama D, mapema wiki hii alionekana kumjibu baba mtoto wake huyo baada ya kuachia picha zake kali akiwa kimahaba na mpenzi wake wa sasa, Shamte ambapo zilizua gumzo kama lote.

Picha hizo zilisambaa kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram ambapo zinamuonesha mama Diamond na Shamte wakilishana keki kimahaba zaidi na watu wao wa karibu kushangazwa na mambo wanayoyafanya wazazi hao kwani hayalingani na umri walio nao.

“Jamani huyu mama naye amekuwa akijiachia mitandaoni kama vijana wa sasa hajui umri wake umeshapita, si awaachie vijana yaani hajishtukii kwamba hakuna wazazi wengine wa mastaa ambao wanafanya haya wanayoyafanya,” aliandika mmoja wa watu wao wa karibu waliokuwa wanatoa maoni kwenye picha hizo.

Wiki iliyopita baba Diamond na Baby Madaha walinaswa kimahaba msituni wakati walipokuwa wamekwenda kufanya utafiti wa kazi zao katika Hifadhi ya Mazingira Asilia ya Magamba iliyopo wilayani Lushoto jijini Tanga ambapo picha zao zilisambaa kila kona.

Hakika leo ni siku ya Ijumaa yenye nuru dhahiri na harufu yenye kutawaliwa na Surat Kahf, kwa uwezo wake Rabbana inshallah! Swala yako ya leo iwe njia ya peponi, Dua zako za leo ziwe kinga ya milele, Udhu wako wa leo uwe shufaa yako milele hadi yaumulkiama. Ameen. Ijumaa kareem…
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mama dai anafikisha miaka 60. ndo maana anafanyiwa birthday kubwa. ila hawataki kusema umri wake.

    ReplyDelete
  2. kweli kabisaa, nakumbuka kwenye birthday yake wakati Domo alikuwa na Wema alisema anamiaka 53. Na alikuwa hajaolewa na kiben ten chake. kudanganya miaka wakati sura unaishindilia marangi ili uonekane kijana nako ni...K

    ReplyDelete

Top Post Ad