Sakata la Sauti Zinazodaiwa za Makada wa CCM Lafika Polisi, TCRA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Fukuto linaloendelea juu ya sauti zinazodaiwa kuwa ni za makada waandamizi wa CCM limefika mbali zaidi kufuatia Jeshi la Polisi kudai kuwa linaanza kufanyia uchunguzi sauti hizo huku huku tayari Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeshasema kuwa tukio hilo ni jinai.

Sauti hizo fupi zilizorekodia kwa njia ya mazungumzo ya simu zinadaiwa kuwahusisha Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye; aliyekuwa waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), January Makamba; makatibu wakuu wastaafu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Yusuf Makamba pamoja na waziri wa zamani wa Mambo ya Nje, Benard Membe.

Msemaji wa TCRA, Semu Mwakyanjala amesema kwamba hiyo ni jinai na wenye mamlaka ya kuchunguza jinai ni Jeshi la Polisi.

“Hii ni jinai na mwenye mamlaka kuchunguza ni polisi, sisi tutawapa ushirikiano wakihitaji na tumekuwa tukifanya hivyo kila wanapohitaji,” Mwakyanjala amenukuliwa na Mwananchi.

Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Simon Sirro amesema bado wanachunguza ili kubaini ukweli. “Hakuna jambo kama hilo linaweza kupita tusilichunguze.”
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad