Viongozi Waliompiga Mshiriki Umiss Pamoja na Kampuni yao Wafungiwa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limeisimamisha Kampuni ya Makumbusho Entertaintment pamoja na viongozi wake kujishughulisha na shughuli yoyote ya masuala ya sanaa na burudani mpaka itakapo amuliwa vinginevyo

Katibu Mtendaji wa BASATA, Godfrey Mngereza amesema wakiwa kama wasimamizi wa shughuli za sanaa nchini wamepokea kwa masikitiko taarifa za unyanyasaji wa Kijinsia uliofanywa na kampuni hiyo dhidi ya mshiriki wa Shindano la Miss Shinyanga 2019, Nicole Emmanuel (19)

Nicole alidai kupigwa na kuchaniwa nguo hadharani na waandaji wa mashindano hayo wa Kampuni ya Burudani ya Makumbusho Entertainment mjini Shinyanga wakati akidai fedha zake nauli shilingi 70,000/= mnamo Julai 6, 2019

Viongozi wa Makumbusho Entertainment wanaotuhumiwa kumpiga na kumdhalilisha binti huyo ni Meneja Mkuu, George Foda na Mkurugenzi, Richard Luhende ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika (SHIRECU) mkoa wa Shinyanga
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad