Waziri wa Afya Ajiuzulu Kisa Ebola

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Waziri wa Afya wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Oly Illunga, amejiuzulu kwenye nafasi yake ya Uwaziri, ambapo ameeleza sababu ya kufanya hivyo ni kutoridhishwa na namna mlipuko wa ugonjwa wa Ebola, unavyoshughulikiwa nchini humo.


Akitangaza kujiuzulu kwake, Ilunga amemshutumu Rais wa nchi hiyo Felix Tshisekedi, kwa kumteua mtu mwingine kuongoza kikosi kinachokabiliana na ugonjwa huo, ambapo kupitia barua yake ya kujiuzulu Illunga amesema nchi hiyo haina nia thabiti ya kupambana na Ebola.

“Kwa sababu ya uamuzi wa Rais Tshisekedi kuweka mikakati dhidi ya virusi vya Ebola chini ya usimamizi wake moja kwa moja, nimejuzulu kama Waziri wa Afya, ilikuwa heshima kuweka utaalam wangu na kuihudumia nchi yangu katika miaka hii miwili ya historia yetu,” ameandika kwenye baria yake

Mapema jana Jumuiya ya Afrika Mashariki, ilitangaza kuwa kutokana na muingiliano mkubwa wa kibiashara kati ya nchi wanachama wa EAC na DR CONGO, upo uwezekano mkubwa wa ugonjwa wa Ebola kusambaa zaidi kutokana mwingiliano wa watu kuzihasa Serikali za EAC kuwa makini na ugonjwa huo.





-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad