Mkandamizaji 'Msimtukane HARMONIZE Kisa anaondoka WCB' '

 

Hakuna Mzazi anayependa mtoto azeekee nyumbani, ni ndoto ya mzazi yeyote mtoto anavyokua basi anamuwezesha ikibidi ili akajitegemee!!

NASSIB (Diamond)

Amefanya kazi kubwa na ya kupongezwa ya kukiona kipaji hiki kilichobezwa na kumsaidia kumfikisha kwenye HARMONIZ wa leo!!

Isitoshe KIWANGO CHA PLATNUMZ Hakitetereki kisa KONDE BOY anaondoka🤷🏾‍♂️ ISITOSHE

NI FAHARI KWA DIAMOND KUONA HATA YULE ALIYE DHARAULIWA KUCHEKWA LEO AMEMFIKISHA KWENYE KIWANGO CHA NYOTA TANO!! (Makofi kwa Platinumz kidogo)

OMBI LANGU KWA WATANZANIA

Msimtukane HARMONIZE Kisa anaondoka WCB Kumbukeni na yeye ni mtafutaji wa kutumia kipaji ambacho kina mda Maalumu na asipotumia wakati vizuri itamgharimu badae!!

HUYU HARMONIZE 

Anatoka kwenye familia ya kawaida kama zetu za hali ya mtu, leo pamoja na kwamba amesaidiwa na yeye anamchango wake kufika hapo alipo hivyo TUSIMKEJERI

Viongozi wa WCB Wanakiri kuwa dogo anaondoka kwa heshima na ameomba wakae mezani na si BASATA ili wapitie mkataba ili naye akajihangaikie mbele kwa mbele KWANINI TUMBEZE MTU MWENYE UTHUBUTU?

Mnataka TUWE na Jamii ya Vijana WAOGA WA FURSA??

Tumemsikia mara kadhaa akisema Diamond ni kama Baba ake kwa namna alivyo msaidia sasa mlitaka azeekee WCB? Kahama mweee wangu LOWASA CCM NA KISHA KARUDI Itakuwa KONDE BOY?

Akishindwa si atarudi ndo maana anaondoka vizuri jamani watanzania!!

Tuweni waungwana, Tusikatishane tamaa, Tuombeane na kutakiana mema.

KUMBUKA HATA WEWE KUNA SEHEMU UNAENDA NA KWA KADRI UNAVYOTUKANA MTU ASIYEKUKOSEA LEO NDICHO UTAKACHOVUNA TENA PENGINE UTATUKANWA KWENYE LEVEL YA CHINI KULIKO KONDE BOY!!

All the best 

MMAKONDE WA CHITOHOLI

 HABARI HIZI ZINAPATIKANA APP YA UDAKU SPECIAL BONYEZA HAPA  

Loading...

Mkandamizaji 'Msimtukane HARMONIZE Kisa anaondoka WCB' ' Mkandamizaji 'Msimtukane HARMONIZE Kisa anaondoka WCB' ' Reviewed by Udaku Special on August 22, 2019 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.