CCM yatoa agizo kwa watendaji wa serikali

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Watendaji wa serikali wametakiwa kutokuwa vikwazo katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na serikali, ikiwemo miradi ya maji na barabara.


Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Ruvuma Odo Mwisho na kulia ni Katibu mkuu wizara ya Maji, Prof. Kitila Mkumbo.

Agizo hilo limetolewa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Ruvuma Odo Mwisho, akiwa na kamati ya siasa ya mkoa kwenye ziara ya ufuatiliaji wa miradi inayotekelezwa na serikali katika wilaya ya Songea mkoani humo.

''Wizara yetu ya Maji imefikia mahala imebweteka sana, serikali inaweza kutenga fedha lakini mpaka mkandarasi azipate fedha hizo inachukua muda, inabidi tukutane na RAS ili atuambie wao kama mkoa tatizo lipo wapi kwasababu jukumu lao ni kuhimiza wizara ilete fedha hizo'', amesema Odo.

Aidha Mwenyekiti huyo, amewataka watendaji wa serikali katika ngazi zote wahakikishe wanasaidia chama hicho kutimizia ahadi zake kwa wananchi ili wasione kama wanadanganywa na serikali yao.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Songea Polilety Mgema, ameuelezea mradi huo wa maji kuwa ni mradi ambao ulianza kutekelezwa muda mrefu na wakandarasi waliondoka eneo la mradi kwa kukosa malipo hata kabla ya awamu ya tano kuingia madarakani.

Mradi huo upo katika kijiji cha Maweso halmashauri ya Madaba Wilayani Songea mkoani Ruvuma.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad