Cristiano Ronaldo afunguka mipango ya kustaafu soka

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mshambuliaji wa Juventus na timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo ameweka wazi hana mpango wa kustaafu soka mwishoni mwa msimu huu wa 2019/20 ama miaka ya hivi karibuni.

Mreno huyo mwenye umri wa miaka 34, ameimbia Fox Sports kuwa, bado na uwezo wa kuendelea kucheza soka kwa kiwango kikubwa cha ushindani hadi akifikia miaka 40.

"Sina mawazo ya kuachana na mpira, pengine naweza kuwa na mawazo hayo nikifikisha miaka 40 au 41, ninauwezo wa kuendelea kucheza. Zawadi ya kipaji nilichonacho natakiwa kuendelea kukifurahia," alisema kwenye mahojiano na kituo cha Tv, Italia.

Aliongeza; "Kuna wanasoka mwenye rekodi zaidi yangu, sidhani kama wapo ambao wanaweza kunizidi."

Ronaldo, ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia wa mwaka mara tano sawa na nyota wa FC Barcelona, Lionel Messi ambaye kwa sasa anasumbuliwa na majeraha.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad