"Hakuna Muujiza wa Kusogeza Magari" - DART

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

"Hakuna muujiza wa kusogeza magari" - DART
Msemaji wa Mradi wa Mabasi Yaendayo kwa Haraka ( DART) maarufu Mwendokasi, Deus Bugaywa amesema foleni iliyokuwepo leo Agosti 14, katika kituo cha mabasi hayo kilichopo Mbezi Mwisho inatokana na kuwepo kwa foleni kubwa ya magari barabarani hali iliyosababisha mabasi kuchelewa kituoni.

Akizungumza na EATV & Radio Digital, Bugaywa amesema foleni ya Mbezi haiwezi kwenda kwa matakwa ya mtu binafsi kwa sababu njia ni moja na inatumiwa na magari ya kawaida na mabasi, hivyo hakuna muujiza wa kuyasogeza ili yawahi kuchukua abiria.

''Mbezi huwezi ukategemea mipango yako kwa sababu ile ni foleni na kuna wakati magari yanakata kabisa, hali ya barabara ndio inatafsiri aina ya huduma zitakayoendelea. Mbezi ni eneo ambalo barabara inatumiwa na magari mengine kwahiyo mfumo wa barabara zingine zitakavokuwa", amesema Buganywa.

"Mfumo utakavyokuwa kama kuna foleni lazima tu magari yatakwama kwenye foleni na hakuna muujiza wa kuyasogeza hapo na hata abiria wanajua na tumekuwa tukiwaelewesha katika hilo'', ameongeza.

Hatua ya kuutafuta uongozi wa DART, imekuja baada ya kushuhudia hali ya foleni ya watu katika eneo hilo,  walioonekana kukaa kwa muda mrefu bila gari kutokea.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad