8/13/2019

Hii Hapa Ndio Talaka Ghali Zaidi Kuwahi Kutokea Duniani..Mke Alamba Mamilion ya Fedha

MacKenzie Bezos ndiye anayeshika nafasi ya tatu katika wanawake matajiri zaidi duniani kwani hitimisho la talaka yake na mumewe anaye miliki Amazon Jeff Bozos hii leo limegharimu hisa za Amazon zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 36.8 ambazo ndio utajiri wa macKenzie kuanzia sasa.

Hii ndiyo takala ghali zaidi diani. Jeff Bezos ambaye ndiye tajiri zaidi duniani ametoa robo ya hisa zake katika kampuni yake ya Amazon na kumpatia mmkewe lakini bado anaendelea kushika nafasi ya kwanza katika watu matajiri zaidi duniani.

Jeff aliahidi hisa hizo tangu mwezi April kuwa atatoa watakapo fikia hitimisho la talaka. Jeff na MacKenzie walifunga ndoa tangu mwaka 1993 ambapo mwaka uliofuata ndipo Jeff alianzisha kampuni yao ya Amazon.

Kwa sasa Jeff mwenye miaka 55 anatajwa kuwa na mahusiano na mwanamama Lauren Sanchez ambaye alikuwa mtangazaji wa habari.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a Comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger