Kuondoka kwa Harmonize WCB tutegemee Mwisho wa Ali Kiba?


Ni siku chache zijazo, tutaanza kuzisikiliza nyimbo za Harmonize bila kibwagizo cha ‘Wasafi Records’ na ‘Eyo Laiza’. Mwanamuziki huyo, ambaye jina lake halisi ni Rajab Abdul Kahali ameandika barua ya kujitoa katika lebo ya Wasafi Records.

Msanii huyo ambaye nyimbo zake za ‘Kwangalu’ na ‘Show Me’ zimeleta gumzo nchini, bila shaka ataleta upinzani mkubwa kwa wasanii wa lebo hiyo akiwamo Diamond mwenyewe.
Kwa sababu Harmonize ameishi WCB, anajua nguvu yao, anajua udhaifu wao, anajua sehemu ya kupita na kufanya vitu vya tofauti.

Licha ya watu wengi kudhani kuwa WCB itatetereka, hali haiwezi kuwa hivyo kwa sababu Diamond na wenzake wataamka na kufanya vitu vya tofauti zaidi wakijua sasa wapo katika mapambano halisi.
Hilo haliwezi kukwepeka kwa sasa kwamba Diamond atajipanga zaidi kwa sababu katika akili yake anajua kuwa Harmonize anakwenda kuwa mpinzani wa kweli tofauti na Ali Kiba, ambaye upinzani wake umetengenezwa zaidi na mashabiki.

Ushindani huo unaweza ukampoteza kwa muda Ali Kiba, ambaye mashabiki wamekuwa wakilazimisha ili aonekane kuwa mpinzani wa Diamond.
Utajiuliza kwanini mashabiki wanalazimisha? Hoja hapa ni kuwa unamlinganishaje msanii ambaye kwa mwaka anatoa nyimbo zaidi ya 10 na mwingine ambaye anatoa wimbo mmoja.

Ni rahisi kutetea kuwa idadi haijalishi, lakini ni ukweli kuwa Diamond anafanya muziki kibiashara tofauti na Ali Kiba, ambaye kwa kiasi kikubwa anafanya kama ‘kujifurahisha zaidi’. Bila shaka mashabiki wa Ali Kiba na wale wanaomchukia Diamond, kwa muda fulani watashangilia chochote kinachofanywa na Harmonize na kila wimbo wa msanii huyo utapendwa na kundi hilo la mashabiki bila kujali kiwango chake.

Kwa namna fulani jambo hilo linaweza kufanya ushindani wa Diamond na Harmonize kuwa mkali kwa muda fulani na hasa itategemeana na jinsi Harmonize atakavyoondoka WCB kama ni kwa shari au kwa amani.

Kwa vyovyole vile, upinzani wa Diamond na Harmonize unaweza kufunika nyota ya Ali Kiba kama akishindwa kucheza karata zake vizuri.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA APP YA UDAKU SPECIAL BONYEZA HAPA  

Loading...

Kuondoka kwa Harmonize WCB tutegemee Mwisho wa Ali Kiba? Kuondoka kwa Harmonize WCB tutegemee Mwisho wa Ali Kiba? Reviewed by Udaku Special on August 25, 2019 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.