Makosa 4 aliyoyafanya Harmonize mpaka sasa


1: Kuruhusu upande wa WCB kutangulia kueleza tofauti yao.

Baada ya Salam SK, kuongea, asilimia kubwa imeshaamini kua Harmo anaondoka WCB kwa jeuri. Kiburi, kujisikia na amekosa fadhila. Itamchukua muda sana kulifuta hili kwenye safari yake. Ukweli hua hauzungumzwi mara mbili.

2: Kumfolow Ali Kiba. 
Bila shaka kichwani Harmonize anawaza ukubwa wake utakavyokua baada ya kuondoka WCB. Kwa vyovyote vile ili aupate ukubwa huo ni lazima apambane kusimama juu ya au kufika pale walipo Kiba na Diamond

Kufika hapo si kwa idadi ya watu wanaosikiliza ngoma zako ila ni kua na idadi kubwa ya watu wako wanaokuamini. Wasanii wengi wameua carear zao kwa kukosa uvumilivu wa kutengeneza mashabiki wao, wengi wamenasa kwenye mtego wa Kiba na Mondi. Ref Baraka da Prince, Rich Mavoko.

Kumfolow Kiba sasa ni ishara ya kutafuta huruma ya upande wa pili. Upande ambao unapambana na upande wa Diamond. Huku anaweza kupata nusu watakaomsapoti lakini lazima ajue kwa upande wa mashabiki wa WCB hakuna atakaemsapoti tena. Ameiweka rehani biashara yake!

3: Kujaribu kuacha 'kivuli chake WCB.' .

Ni vyema kuonekana bado anaipenda WCB, lakini kwa faida ya kazi yake na aina ya mashabiki tulionao, Harmo hatakiwi kuihusisha kazi yake na WCB. Kufanya hivyo huenda hili likawa kaburi lake kimuziki.

Kuna dhana ya unafki itaanza kumtafuna. Kama alifuta ile kusainiwa WCB, hakukuwa na ulazima wa kuacha neno WCB for Life kwenye Bio yake. Kwa lugha ya Salam SK, Harmo alianza kuivimvimbia menegament yake kabla ya kutoka. Hakuna anayejua nyuma ya kicheko cha Diamond, kuna nini.

4: Kutaka kuachia wimbo mpya haraka
Hili ni kosa kubwa sana. Saa chache baada ya Salam SK kuongea, Harmo amepost cover kua yuko mbioni kuachia ngoma. Hii ni tension mbaya sana anaitengeneza.
Kwa sababu ya presha ya hivi sasa, wako watakaoichukia kazi yake. Haijalishi ubora wake, Liko sikio litamkataa tu kwa kuonekana ana kiburi cha kushindana.

Iko dhana ya 'KIKI' pia inaweza kuingia. Akaonekana mtu wa drama za mitandao. Hii ni mbaya sana.

NB: Pengine Harmo hajajua kua ni ngumu kuitofautisha WCB na Diamond. Ajipange kwa yote.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA APP YA UDAKU SPECIAL BONYEZA HAPA  

Loading...

Makosa 4 aliyoyafanya Harmonize mpaka sasa Makosa 4 aliyoyafanya Harmonize mpaka sasa Reviewed by Udaku Special on August 23, 2019 Rating: 5

5 comments:

 1. Mwandishi WA hii makala nnavyo ona mimi NI kwamba ametumwa au anatumiwa au NI miongoni WA yote.

  Huyu utumbo aliouandika nadhani ingekuwa vyema kuzungumza kijiweni na Wana kiniwe kama Ina man ufaa kwao na siyo kwenye blog yetu hii ya Udaku.

  Kuendelea MBELE KATIKA utafutaji na kujiamini NI kitu Cha kawaida.

  Na alicho fanya Konde boy ujue Vanny boy pia yuko njiani akifatiwa Dimond I mwenyewe na Marombosso pia. Na hata lava lava.

  Wasafi atabaki Salam manake HATA tale tale atamfata dimondi kama hujui yanayoendelea Wasafi na mpangilio WA Menejimenti ya mtu mmoja.

  Tunakuombea kama huwe kumpa moyo Konde boy..!! KAA KIMYA

  ReplyDelete
 2. Mwandishi WA hii makala nnavyo ona mimi NI kwamba ametumwa au anatumiwa au NI miongoni mwa yote.

  Huyu utumbo aliouandika nadhani ingekuwa vyema kuzungumzia kijiweni na Wana kijiwe kama Ina manufaa kwao na siyo kwenye blog yetu hii ya Udaku.

  Kuendelea MBELE KATIKA utafutaji na kujiamini NI kitu Cha kawaida katika Maisha

  Na alicho fanya Konde boy ujue Vanny boy pia yuko njiani akifatiwa na Dimondi mwenyewe na Marombosso pia. Na hata lava lava.

  Wasafi atabaki Salam. manake HATA tale tale atamfata dimondi kama hujui yanayoendelea Wasafi na mpangilio WA Menejimenti ya mtu mmoja.

  Tunakuomba kama huwezi kumpa moyo Konde boy..!! KAA KIMYA

  ReplyDelete
 3. Mwandishi WA hii makala nnavyo ona mimi NI kwamba ametumwa au anatumiwa au NI miongoni mwa yote.

  Huyu utumbo aliouandika nadhani ingekuwa vyema kuzungumzia kijiweni na Wana kijiwe kama Ina manufaa kwao na siyo kwenye blog yetu hii ya Udaku.

  Kuendelea MBELE KATIKA utafutaji na kujiamini NI kitu Cha kawaida katika Maisha

  Na alicho fanya Konde boy ujue Vanny boy pia yuko njiani akifatiwa na Dimondi mwenyewe na Marombosso pia. Na hata lava lava.

  Wasafi atabaki Salam. manake HATA tale tale atamfata dimondi kama hujui yanayoendelea Wasafi na mpangilio WA Menejimenti ya mtu mmoja.

  Tunakuomba kama huwezi kumpa moyo Konde boy..!! KAA KIMYA

  ReplyDelete
 4. Namkubali sana Konde Boy maana kwanza nyimbo zake siyo Love oriented sana kwahiyo ni mtu wa kutufunza mambo mengi

  ReplyDelete
 5. WCB ni Uhuni mtupu kuumizana kimuziki na unyanyapaa ni kitu cha kawaida huko

  ReplyDelete

Powered by Blogger.