8/13/2019

Mengine yakufahamu kuhusu DJ Arafat kabla ya umauti kumfika

Mengine yakufahamu kuhusu DJ Arafat kabla ya umauti kumfikaMoja ya taarifa kubwa ya simanzi iliyoripotiwa siku ya jana August 12, 2019 ni hii ya kifo cha msanii maarufu nchini Ivory Cost Ange Didier Houon maarufu kama DJ Arafat aliyefikwa na umauti kutokana na ajali ya kugongana na gari wakati akiendesha pikipiki.

DJ Arafat amefariki akiwa na umri wa miaka 33 na alipata umaarufu sana kutokana na style yake ya kipekee kwenye muziki ambayo amekuwa akiifanya na hata kushirikishwa kwenye kolabo mbalimbali na wasanii tofauti tofauti ndani ya bara la afrika.

Mpaka umauti unamfika DJ Arafat alikuwa ni miongoni mwa wasanii waliokuwa wanawania tuzo ya Afrimma kupitia kipengele cha BEST FRANCOPHONE ambacho kilikuwa kikiwaniwa pia na wasanii kama Fally Ipupa, Toofan, Ya Levis na wenginewe.Pamoja na halo pia marehemu DJ Arafat alifanya kazi kibao ambazo zilipata umaarufu kama Yorobo, Ventiprontent na hata Touch Body aliyoshirikishwa na J. Martins huku akiwa ameacha sokoni album kumi na moja.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger