Ripoti kamili kuhusu ndege iliyoteketea Mafia leo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Kamanda wa Polisi kanda Maalumu ya Rufiji  Onesmo Lyanga, amethibitisha kutokea kwa ajali ya ndege ndogo ya shirika la Tropical, iliyokuwa ikiruka kutoka katika kiwanja cha ndege cha Mafia kuelekea Dar es Salaam.


Kamanda wa Polisi kanda Maalumu ya Rufiji  Onesmo Lyanga.

Kamanda Lyanga amesema ajali hiyo imetokea leo Agosti 6 majira ya saa 4:00 asubuhi, baada kuanguka na kuteketea kwa moto na ilikuwa na abiria  takribani tisa.

''Ndege imepata ajali ilikuwa inaruka uwanja wa Mafia kwenda uwanja wa Julius Nyerere Dar es salaam, ilikuwa na watu 9 lakini mpaka sasa hivi hakuna aliyefariki na kuna majeruhi 6 na ndege yote imeteketea.

Aidha kamanda amesema kuwa majeruhi wote 6 wamekimbizwa hospitali kwa ajili ya matibabu zaidi na kwamba Jeshi la polisi Mkoani humo linaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo cha ajali hiyo.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad