Nabii Mwanamke Bilionea wa Kutupwa Atikisa Bongo...Unaambiwa Anatembea na Mabodigadi Diamond Hafiki


NI kishindo cha aina yake! Nabii mwanamke, Dk Lucy Natasha ambaye ametinga Bongo kufanya huduma katika makanisa mbalimbali, ameibua gumzo mjini baada ya Wabongo kufahamu habari zake, Ijumaa Wikienda limekukusanyia habari kamili.

Dk Lucy ambaye ni mwanzilishi wa huduma ya kinabii ya Ministries International ya nchini Kenya, alitua Bongo wiki iliyopita ambapo mara baada ya kukanyaga Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar, watu walianza kumjadili kutokana na muonekano na mafanikio yake. “Mh! Huyu nabii si mchezomchezo, angalia msafara wake ulivyo mkubwa, angalia ulinzi, magari yake na ninasikia huko kwao Kenya ni tajiri kwelikweli, anamiliki magari na majumba ya kifahari,” alieleza mmoja wa watu walioshuhudia ujio wake.

Ijumaa Wikienda lilijaribu kuzungumza na mmoja wa wenyeji wa mchungaji huyo ambaye hakupenda jina lake lichorwe gazetini ambaye alifunguka mambo mengi kuhusu huduma na utajiri wa nabii huyo. “Huyu nabii ni maarufu sana Kenya na nchi mbalimbali kama vile Afrika Kusini, Rwanda, Burundi na kwingineko duniani kwani anatoa hudumu katika nchi zaidi ya 50. “Ana kipawa cha ajabu sana, alianza kuhubiri akiwa na umri wa miaka tisa akiwa shule ya msingi. Amekua hivyohivyo akihubiri na bahati nzuri mama yake pia alikuwa mchungaji, akasoma na kuhitimu masomo ya Biblia na sasa ni nabii. .

GUMZO KILA KONA

“Amekuwa maarufu zaidi kupitia huduma zake anazofanya kwani anafanya kama semina katika nchi mbalimbali, anafundisha Biblia na anafundisha elimu ya maisha hivyo amekuwa akiwagusa wengi. Anapata mialiko mingi sana na ndiyo maana umeona amekuja pia nchini,” alisema.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA APP YA UDAKU SPECIAL BONYEZA HAPA  

Loading...

Nabii Mwanamke Bilionea wa Kutupwa Atikisa Bongo...Unaambiwa Anatembea na Mabodigadi Diamond Hafiki Nabii Mwanamke Bilionea wa Kutupwa Atikisa Bongo...Unaambiwa Anatembea na Mabodigadi Diamond Hafiki Reviewed by Udaku Special on August 25, 2019 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.