Natoa kauli hii sio kuwatisha, Serikali ya Magufuli haiwezi kuchezewa na yeyote - Waziri Lugola

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Tanzania na Burundi wamesaini makubaliano ya kuwarejesha Wakimbizi 2000 kwa kila wiki nchini mwao kuanzia Oktoba Mosi, 2019.

Wakimbizi hao waliopo katika Kambi ya Nduta na Mtendeli wanatarajiwa kusafirishwa kuelekea katika nchi yao ya asili kutokana na amani iliyopo katika nchi hiyo.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, na Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchini Burundi, Pascal Barandagiye tayari wamesaini makubaliano hayo ambayo watahakikisha wakimbizi wote waliopo katika kambi hizo wanartejeshwa nchini mwao bila kukwamishwa na mtu au
shirika lolote.

Akizungumza na waandishi wa habari, mjini Kigoma jana, Waziri Lugola alisema makubaliano hayo yataanza rasmi Oktoba mosi na wakimbizi hao watakuwa wanarejeshwa nchini mwao na kupata mapokezi makubwa na Serikali ya Burundi.

“Tunataarifa wapo baadhi ya watu, mashirika ya kimataifa wanawarubani wakimbizi wakiowatangazia kuwa Burundi haina amani, jambo ambalo si la kweli, nchi hiyo ina amani na wakimbizi wanapaswa kurejea nchini mwao,” alisema Lugola.


Lugola aliongeza kuwa, atawachukulia hatua kwa watakaokwamisha zoezi hilo la kuwasafirisha wakimbizi hao, kwa kuwa Serikali ya Wakimbizi inataka watu wao na Tanzania imeamua kuwapa watu wao ili waende wakaijenge nchi.

“Natoa kauli hii sio kuwatisha au kutishia nyau, bali nasema, Serikali ya Magufuli haiwezi kuchezewa na mtu yeyote, hivyo tutawakamata wanaowarubani, wanaowashawishi wakimbizi wasiende nchini mwao,” alisema Lugola.

Wiki iliyopita, katika mkutano wa hadhara katika Kambi ya Nduta, baadhi ya Wakimbizi walisema wanawekewa vikwazo na kucheleweshwa na baadhi ya watendaji wa mashirika ya wakimbizi kambini humo wakati wanapoomba kujiandikisha kurejeshwa kwao.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad