8/16/2019

Polisi Yavamia Mkutano wa Zitto, Yamkamata Msemaji ACT

Jeshi la Polisi limevamia makao makuu ya chama cha ACT Wazalendo yaliyopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam na kuzuia mkutano wa Kiongozi Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe, aliokuwa aufanye leo Ijumaa, Agosti 16, 2019 na wanahabari ofisini hapo.
Polisi pia, wamemkamata Katibu wa Uenezi wa chama hicho, Ado Shaibu,  na kuelekea naye kituo cha Polisi Oyster Bay, jijini Dar es Salaam kwa mahojiano.

Naibu Katibu wa Uenezi ACT Wazalendo, Seif H. Suleiman,  amethibitisha tukio hilo na kusema magari mawili ya askari polisi wakiwa na silaha walifika ofisini hapo na kuzuia mkutano huo ambapo dakika takribani 15, waliondoka na Ado Shaibu.
Leo, Zitto Kabwe alitarajia kuongea na waandishi wa habari kuhusu Mkutano Mkuu wa 39 wa Wakuu wa Nchi za Jumuia ya Maendeleo ya Nchi za Kusdini mwa Afrika (SADC).
Mkutano huo umeahirishwa mpaka taarifa nyingine zitakapotolewa.

TAZAMA ALICHOFANYA ROSA REE BAADA YA KUFUNGULIWA NA BASATA

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

4 comments:

 1. Bado tu usumbufu wa vyombo vya dola kwa vyama vya upinzani haujaisha.

  ReplyDelete
  Replies
  1. Mdau, Kwa akili zako Huu ni wakati muafaka kwa Huyu anae jiita Kiongozi Mkuu ya hicho chama kutaka kuzungumzia Kongamano Jumuishi la SADC.. Ama kweli punguwaani ni wengi…!!!

   Zitto Rudi kwenu.. Uhakiki unaendelea katika Idara Za Uhamiaji ni Bora ukusha maliza Kesi inayo kukabili ukafunga Virago... Tumekuchoka.

   Delete
 2. Zitto Ruyagwa Zuberi Kabwe! Nikuulize, Je unatafuta Ajira aliyopewa Dkt Abbasi..!!!!

  nanuku …. ( Leo, Zitto Kabwe alitarajia kuongea na waandishi wa habari kuhusu Mkutano Mkuu wa 39 wa Wakuu wa Nchi za Jumuia ya Maendeleo ya Nchi za Kusdini mwa Afrika (SADC).
  Mkutano huo umeahirishwa mpaka taarifa nyingine zitakapotolewa).  Hivyo huna hata Haya na Haiba.. Kujivisha Kilemba cha Ukoka..??


  Wewe wapi na Mkutano huu wapi?? Au unajifanya Makonda??

  Sasa Mwaya Kwa Taarifa yako na wenye mwelekeo kama wako wa Usindikizaji na Ucheleweshaji ulio kithiri. Tuna kuomba na Kukukanya. YASIYO KUHUSU USIJIINGIZE INGIZE. TUKUKUTAKA TUTAKUALIKA NA SI VINGINEVYO.. WANA HABARI UZALENDO NA TASWIRA YA NCHI YETU KWA WAKATI KAMA HUU NA UGENI HUU NDIYO KIPA UMBELE KULIKO USHABIKI WA HAWA WANAO JIITA WANA SASA MCHWARA. NI WA KUPOTEZEWA NA MAHOJIANO NA UCHUKUZI WA TAARIFA ZAO UTAFANYWA NA VYOMBO HUSIKA.

  ReplyDelete
 3. KICHWA SAHIGI CHA HABARI NI KAMA ILIVUO HAPO CHINI.

  POLISI KANDA MAALUM KTK DORIA WATAWANYA MKUSANYIKO AKIWEMO ADO SHAIBU AMBAE ATASAIDIA MAELEZO KITUONI.

  VICHWA VYA HABARI NI LAZIMA VIWE MAKUNI NA MAUDHUIA,
  NAOMBA BAADHI YA WAANDISHI NA WAHARIRI WAPELEKWE URUSI NA UCHINA KUJIFUNZA HAYA YA KURIPOTI NA KUHABARISHA MA KWA MANUFAA YA NCHI.

  ReplyDelete

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger