Serikali Yaunda Kamati Maalumu ya Kushughulikia Waliofariki Kwa Ajali ya Moto Morogoro

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Waziri wa  Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu), Jenister Mhagama amesema Serikali imeunda kamati ya wataalamu itakayotambua maiti na majeruhi waliotokana na ajali ya lori la mafuta lililopinduka leo Jumamosi mkoani Morogoro na kulipuka.

Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la ajali leo,  Waziri Mhagama amesema baadhi ya mawaziri watakuwa na vikao mkoani humo kujadili jinsi ya kumaliza msiba huo.

Amesema Kuna timu ambayo imeshaanza kufanya ‘assessment’  ya namna ya kuhifadhi  waliofariki kwa namna yoyote ile ili ambao hawatatambuliwa serikali ya Mkoa wa Morogoro ione nini cha kufanya..

Mkuu wa wilaya ya Morogoro Mjini, Mary Chonjo amesema kuanzia kesho Jumapili saa 2 asubuhi watanza kutambua miili na kuwataka wananchi waliojitokeza kutambua ndugu zao kutawanyika.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad