google-site-verification: googleb0bc30c3e5fdb812.html Uwanja wa ndege wafunguliwa tena, kiongozi aonya Hong Kong huwenda ikatumbukia shimoni | UDAKU SPECIAL

Uwanja wa ndege wafunguliwa tena, kiongozi aonya Hong Kong huwenda ikatumbukia shimoni

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Baada ya maandamano hapo jana uwanja wa ndege wa Hong Kong umeruhusu tena safari za ndege. Kiongozi wa kisiwa hicho Carrie Lam ameonya kuwa Hong Kong inaweza kutumbukia shimoni ambako itakuwa vigumu kujitoa.

Hongkong Proteste gegen China PK Carrie Lam (Reuters/T. Peter)

Shughuli kwenye uwanja wa ndege wa Hong Kong ambao ni miongoni mwa viwanja vinavyohudumia wasafiri wengi zidi duniani, zimeanza tena taratibu asubuhi ya leo, lakini mamlaka ya uwanja huo imeonya kuwa baadhi ya safari zinaweza kuendelea kutatizwa. Tangazo la kurejesha safari za ndege limewekwa kwenye huduma ya simu za mkononi, au app ya uwanja huo mnamo saa kumi na mbili asubuhi saa ya Hong Kong.

Uwanja huo ulikuwa umeahirisha safari zote za ndege jana Jumatatu, baada ya maelfu ya waandamanaji kukusanyika katika ukumbi wanakofikia wasafiri. Wengi wa waandamanaji hao wameondoka usiku wa kuamkia leo, wakibaki wapatao 50 tu.

Hongkong Proteste gegen China - Generalstreik Flughafen (picture-allaince/AP/Royston Chan)Safari zote za ndege ziliahirishwa jana katika Uwanja wa Hong Kong

Shirika la habari la Reuters limeripoti kuwa wasafiri wapatao 100 walikuwa wamepiga msitari kwenye ofisi ya shirika la ndege la Cathay Pacific asubuhi ya leo. Shirika hilo rasmi la Hong Kong limetishia kuwafukuza wafanyakazi wake watakaobainika kuunga mkono waandamanaji.

Onyo kuhusu athari mbaya kwa Hong Kong

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Wakati hayo yakijiri, kiongozi wa Hong Kong anazongwa na shinikizo, Bi Carrie Lam ametetea mienendo ya polisi katika kukabiliana na mandamano, ingawa miongoni mwa malalamiko ya waandamanaji hao ni jinsi polisi wanavyotumia nguvu za ziada kukandamiza vuguvugu lao. Lam pia ametoa mwito kwa kila mmoja kujizuia kufanya fujo.

”Hebu tumia dakika moja kufikiria jiji letu. Mnataka kulitumbukiza shimoni na kulivunja vipande vipande? Tunahotakiwa kufanya hivi sasa ni kujiepusha na ghasia na kuheshimu sheria,” amesema Lam na kuongeza kuwa baada ya kurejeshwa kwa hali ya utulivu, ndipo ”tunapoweza kuanza mjadala wa kumaliza mgawanyiko katika jamii.”
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad