WIZI MPYA: Ng’ombe waibwa kwa kutumia bodaboda, DC Serengeti atoa agizo


Katika hali ya kushangaza baadhi ya wakazi wa wilaya ya Serengeti mkoani Mara wamekuwa wakilala nje kulinda mifugo yao, Hii ni baada ya kuwepo kwa wezi usiku wanaotumia Pikipiki kuiba mifuko yao.

Wakiongea kwenye kikao cha Baraza la Madiwani katika Wilaya ya Serengeti, Baadhi ya Madiwani wilayani humo wamesema kumekuwepo na matukio ya wizi wa mifugo, kunakofanywa na baadhi ya wananchi katika Wilaya hiyo, hali inayopelekea baadhi ya wananchi kutojikita zaidi kwenye shughuli za maendeleo na badala yake wanakesha kulinda mifugo yao.

“Hatuwezi kujadili maendeleo wakati kuna vitendo vya kihalifu vya wizi wa mifugo na haipiti siku hujasikia mifugo haijaibiwa kwenye eneo hili, kinachoshangaza zaidi ni wezi wanaiba ng’ombe na wanawabeba kwenye pikipiki, lazima tufanye kitu kwa niaba ya wananchi wetu.” amesema Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, Juma Porini.

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Nurudin Babu, ambaye ndie mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama. Ametoa onyo kali kwa wezi hao na kuagiza kuwa Kijiji kitakachobainika kuiba Ng’ombe basi wananchi wake watalipa ng’ombe hao.

“Tayari nimeshaagiza endapo Ng’ombe wataibiwa kwenye Kijiji fulani,  wafuatilie nyayo na endapo watabaini hadi Kijiji alipoelekea huyo ng’ombe basi hicho Kijiji kitalazimika kulipa.” amesema Nurudin Babu.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA APP YA UDAKU SPECIAL BONYEZA HAPA  

Loading...

WIZI MPYA: Ng’ombe waibwa kwa kutumia bodaboda, DC Serengeti atoa agizo WIZI MPYA: Ng’ombe waibwa kwa kutumia bodaboda, DC Serengeti atoa agizo Reviewed by Udaku Special on August 25, 2019 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.