9/17/2019

Afariki kwa Kuchomwa Kisu Akidai 1500


Mtu mmoja amefariki dunia kwa kuchomwa kisu baada ya kudai 1500 kama malipo yake.


Mtu huyo aitwaye Rajabu Abdalah amefariki dunia katika tukio hilo lililofanyika Kata ya Babati wilaya ya Babati mkoani Manyara, baada ya mwenzake kumchoma kisu chini ya titi la upande wa kushoto wakiwa wanagombania shilingi 1500.

Imeelezwa kuwa kiasi hicho cha fedha walipewa na abiria kama malipo baada ya kumbebea mzigo wake kuupeleka katika stendi ya magari.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, kamanda wa polisi mkoa wa Manyara, Agustino Senga, amesema kuwa kutokana na opereseheni kubwa iliyofanyika kumsaka kijana Cleophace John a.k.a Mgogo aliyefanya mauaji hayo walifanikiwa kumpata.

''Tumefanya msako mkubwa na kumkamata  mtuhumiwa aitwaye Cleophace John au maarufu Mgogo, akiwa ndani ya gari aina ya Emmigrace leo Asubuhi ya Septemba 17, 2019 akiwa anajaribu kutoroka kuelekea jiji la Dodoma'', ameeleza RPC. 

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya mji Mrara, ukisubiri uchunguzi wa daktari, huku mtuhumiwa akiwa mikononi mwa polisi  kwa mahojiano zaidi.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger