9/17/2019

Alichokisema Prof Jay kuhusu Kauli ya Paul Makonda


EATV & EA Radio Digital leo, tumezungumza na Mbunge anayesimamia watu na wanyama katika jimbo la Mikumi Mh. Prof Jay, ambapo ametoa maoni kuhusu kauli ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mh. Paul Makonda kuwa watumishi wa Mungu wahubiri hadi kwenye kumbi za starehe."Ngoja tuone kwanza ianze halafu baadaye ndiyo tutajua tuta-comment kitu gani kitakachoendelea lakini kwa mimi sioni kama itaenda kufanikiwa kwa sababu bahati nzuri au mbaya mkuu wetu wa mkoa amekuwa anaongea vitu vingi sana ambavyo havitekelezeki sasa nataka nione kwa hili amaejipangaje".

Prof Jay ameendelea kusema tunaweza kubeza kama haiwezekani baadae akafanikiwa ngoja baada ya muda tuone ana mipango gani na sasa hivi dunia imebadilika unahitaji kupata neno la Mungu mahali popote ila kwenye klabu itakuwa shuguli nzito sidhani kama linawezekana. amesema Prof Jay.

Aidha Prof Jay ameachia kazi yake aliyoshirikiana na ndugu zake wawili Black Rhyno, Donkoli, Mr Teacher na Simple X iitwayo kaza.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

2 comments:

 1. Huyyu black Rhino ni ndugu yake Faru John..?

  Na Yule aliyesilimu sijui Faru Rajabu?
  Sasa mmewaachilia Miumi au Selous?

  Plofesa .J. wewe mwindaji una leseni?
  Halali au...?

  ReplyDelete
 2. Huyyu black Rhino ni ndugu yake Faru John..?

  Na Yule aliyesilimu sijui Faru Rajabu?
  Sasa mmewaachilia Mikumi au Selous?

  Plofesa .J. wewe mwindaji una leseni?
  Halali au...?

  ReplyDelete

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger