Alichosema Dkt Benson Bana Baada ya Kuteuliwa na Rais Magufuli

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mhadhiri wa Sayansi ya Siasa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dkt Benson Bana ameonesha ni kwa namna gani amefurahishwa na uteuzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli baada ya kumteua kuwa Balozi.

Akizungumza na EATV&EA Radio Digital, dakika kadhaa mara baada ya kutangazwa kuteuliwa kwake, Dkt Bana amesema taarifa hizo amezipata akiwa ndani ya gari lake na amepanga kwenda Kanisani kumshukuru Mungu.

''Sikutarajia kwahiyo ni furaha kubwa, kila kitu kinachotokea Mungu anakusudio lake, nimezipata nikiwa barabarani nikiwa naendesha gari yaani hadi sasa hivi kuna watu kama 30 wamenipigia simu, natafakari maisha baada ya tukio hilo, ngoja nitafakari niende kanisani nikasali kidogo na nikashukuru Mungu basi'', amesema Dkt Bana.

Uteuzi huo wa Dkt Bana umetangazwa leo Septemba 20, 2019 na Katibu mkuu kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad