Amber Lulu ajibu kuhusu ulevi, kuringa kisa umbo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Amber Lulu amepiga stori na EATV & EA Radio Digital leo, ambapo amefunguka juu ya suala la kupewa sifa ya kuwa msanii wa kike anayependa pombe pamoja na kuringia makalio.


Akizungumzia kuhusu sifa ya unywaji wa pombe na ulevi kupitiliza, Amber Lulu amesema kuwa watu wanamzushia masuala yasiyofaa kwani hawakuwahi kumuona sehemu yoyote wala hakuna video inayomuonesha katika hali hiyo.

“Huo ni uongo, watu wengine wanakuaga na chuki tu, kuna muda inatokea huna kazi na upo kwenye 'mood' unahitaji ku-enjoy na mtu anaweza akakuona mara moja akachukulia kama ndiyo maisha yako ya kila siku na hakuna ambaye hanywi”, amesema Amber Lulu.

Aidha Amber Lulu amewajibu wanaomsema kwamba anaringia makalio kutokana na picha anazopost Instagram, akisisitiza kuwa anaringia kila kitu ambacho amejaaliwa na Mungu kama kipaji, nidhamu na uzima wa afya aliopewa.

"Mwili wangu ni wa kawaida kwa sababu ni 'original' huu. Wengine wanatengeneza makalio kwa mchina na wengine wanavaa taiti za maboksi ili waonekane wana makalio makubwa ila
kama mtu ana 'original' inajulikana tu", ameongeza.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad