9/21/2019

Celine Dion Ampa Onyo Drake

Kwa mujibu wa Billboard, Drake aliwahi kuweka wazi kuhusu mpango wake wa kujichora tattoo yenye sura ya muimbaji  CelineDion. Septemba 18 kwenye interview na iHeratRadio, Staa huyo wa Dion  alimtaka Drake kuachana na mpango huo kwani hauna manufaa yeyote.”Usifanye hivyo” aliongea kwa msisitizo. “Unaweza kuandika barua za upendo, unaweza kunitumia autograph kwa ajili ya watoto wangu, unaweza kunitembelea. Naweza kukualika nyumbani kwa ajili ya chakula cha mchana au usiku. Tunaweza kuimba pamoja. Chochote unachotaka hata kama ni kuongea na mama yako ili nikufurahishe”.Celine Dion amesema sura yake inabadilika jinsi muda unavyokwenda wala sio kitu kilichokuwa kikitengeneza hela kwenye fani yake, anaamini tattoo yake kwenye mwili wa Drake haitakuwa na mwisho mzuri na kumfanya Rappa huyo awe na muonekano wa ajabu atakapozeeka.Drake anasifika kwa mahaba yake ya ajabu kwani kila anapomuelewa mtu huamua kuichora sura ya muhusika kwa mfumo wa tattoo. Rihanna, LilWayne, Aaliyah na Sade ni miongoni mwa wanamuziki ambao Drake amewachora sura zao mwilini mwake.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger