Hivi Ndivyo Kim Kardashian Alivyoingiza Bilion 4.5 Ndani ya Dakika Chache..Kuna Watu Wana Mihela Jamani

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Utajiri wa Familia isiyoishiwa na vituko ya The Kardashian sio tu Mamilioni ya watu ambao wanawafatilia kila mahala bali ni ushawishi walionao kwa hao watu, Inaripotiwa Kuwa Kim Kardashian Siku ya Jana (Sept. 10) ameingiza zaidi ya Tsh. Billion 4.5 ( $ 2M) Ndani ya dakika chache tu baada ya bidhaa zake mpya za nguo (SKIMS) kuanza kuuzwa.

Bidhaa hizo mpya ndani ya siku moja tayari zimetajwa kuwa tishio kwa makampuni makubwa ya nguo za ndani za wanawake, Kampuni maarufu ya Spanx ilipata faida ya Dola Million 4 Mwaka wao wa Kwanza Lakini Kim K Tayari ameshaitengeneza nusu ya hizo Pesa ndani ya Dakika Tu. Hata Hivyo haishangazi sana ukiangalia na idadi ya watu wanaomfata kwenye Mitandao ya Kijamii, Kim K ana idadi ya Follower Million 147 Kwenye Instagram na Million 61.5 Kwenye Mtandao wa Twitter.

TMZ wameripoti kuwa kabla ya #KimKardashian kuziachia rasmi hizo bidhaa za nguo za wanawake alilazimika kusogeza mbele hadi siku ya Jumanne (Septemba 10) kutokana na Mtandao uliotakiwa kuuza hizo bidhaa kutembelewa na idadi kubwa ya watu hadi ukaelemewa (Crash) kabla hata hazijatoka, Inaripotiwa kuwa bidhaa hizo ambazo bei yake si chini ya Tsh. 230,000 ziliisha (Sold Out) ndani ya dakika chache tu baada ya kuanza kuuzwa.

HataHivyo Hii sio Mara Ya Kwanza Kwa mwanafamilia wa The Kardashian Kumaliza bidhaa zao sokoni asubuhi tu, Mwezi wa Tano Kylie Jenner aliuza bidhaa zake zote za “Kylie Jenner Skin” ndani ya Dakika 6 tu.
TAZAMA WIMBO MPYA WA ROSA REE

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad