Maagizo ya Rais Magufuli, yamtesa Makonda

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Ikiwa ni siku kadhaa zimepita tangu Rais Magufuli, kutoridhishwa na utekelezwaji wa baadhi ya miradi ya Mkoa wa Dar es Salaam, ikiwemo machinjio ya Vingunguti, imepelekea Mkuu wa Mkoa huo Paul Makonda, kushiriki katika ujenzi wa machinjio hayo hadi nyakati za usiku.


Makonda ameyasema hayo usiku wa kuamkia leo Septemba 22,2019 wakati akishirikiana na Makandarasi waliopewa tenda ya ujenzi wa machinjio hayo ya kisasa, ambapo amesema sauti ya Rais Magufuli kuhusu ujenzi huo, imekuwa ikimfuata mara kwa mara hivyo ameona si vyema kumuangusha.

"Nimeamua kusimamia mwenyewe sababu moja tu niliowaamini nakuwaachia kazi hii wameniangusha na ile sauti ya Rais Magufuli, kuwa nimekubali hii miradi ishindikane, isitekelezeke?, nakuambia Rais na Watanzania wote miradi hii ntaisimamia mwenyewe usiku na mchana ili kuhakikisha ndoto uliyonayo katika mMoa wetu inatimia, sitakuangusha" amesema Makonda.

Makonda amesema kwa sasa hatokuwa akipatikana ofisini, badala yake atakuwa akipatikana 'site' hadi miradi hiyo itakapokamilika.

Machinjio hayo yanatarajiwa kukamilika katika kipindi cha ya miezi 3 ijayo.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad