9/17/2019

Makonda: Kama Siyo Njaa Ningejiuzulu


Dar es Salaam. Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam nchini Tanzania, Paul Makonda amesema kama siyo njaa angejiuzulu nafasi yake ya ukuu wa mkoa ili kuwajibika baada ya Rais John Magufuli kulalamikia ucheleweshaji wa miradi ya ujenzi ya Coco Beach na machinjio ya Vingunguti.

Makonda ameyasema hayo leo Jumanne Septemba 17, 2019 jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kuwadhamini wanafunzi wa kike 100 wa kidato cha tano wanaosoma masomo ya sayansi lakini wazazi wao hawana uwezo wa kuwasomesha.

Kauli hiyo ya mkuu wa mkoa ameitoa ikiwa ni siku moja baada ya Rais Magufuli kumtaka ahakikishe miradi hiyo yenye thamani ya Sh26.47 bilioni inakamilika kwa wakati kwa sababu tayari fedha zipo.

Amesema jana alipata aibu wakati Rais Magufuli alipotembelea machinjio ya Vingunguti na kulalamikia ucheleweshaji wa miradi ya maendeleo katika mkoa wake licha ya vikao vingi ambavyo amekuwa akifanya na watendaji wa halmashauri na kuagiza kuanza kwa miradi hiyo.

“Jana ilikuwa ni aibu, yaani kwa sababu njaa ni kali, kama siyo njaa leo ilitakiwa niandike barua ya ku-resign (kujiuzulu).”

“Sasa nikifikiria njaa iliyopo huko...naomba sana kila mmoja atimize wajibu wake, ukikwama sehemu waone mamlaka ya juu yako, sio unakaa tu,” amesema Makonda.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

1 comment:

 1. Na ndiyo kauli aliyosema Mkuu wetu
  kwa wenye Uelewa na Kuelewa.

  Akimaanisha hakuna cha kutuzuia katika kufikia malengo na Mikakati tuliyo jipangia.

  Na mwisho wake akatumia Neno Kelele za Chura hazi fanyi ng'ombe kuto kunywa maji.

  Kwa hivyo mjipange ..kwani kwa JPM kutumbua si ajabu na asiye weza kkasi yetu...ATUPISHE.

  ReplyDelete

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger