Meneja wa Harmonize Apinga Kuwepo kwa Harusi ya Nyota Huyo na Sara

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Meneja wa msanii Harmonize, Beauty Mmari almaarufu kama Mjerumani, amepinga kuwa nyota huyo alifunga ndoa na mpenziwe Sarah Michelloti mnamo Ijumaa, Septemba 7 Picha za staa huyo wa wimbo maarufu wa 'Kadamshi' na mchumba wake aliyekuwa amevalia gauni lililoashiria wawili hao walikuwa wanafunga ndoa zilisambaa mitandaoni huku maelfu ya mashabiki zake wakimpongeza.

 Kwa mujibu wa Nyakati.com, baadhi ya wafuasi wao mitandaoni walishangaa ni vipi nyota huyo alifanya harusi kisiri pasi na hata kuwaalika wasanii tajika kutoka Tanzania. Hata hivyo, meneja wa Harmonize, Mjerumani amepinga kwamba wawili hao walifunga ndoa na kusema kwamba Sarah alikuwa akiigiza katika wimbo ambao staa huyo anatarajia kuutoa hivi karibuni 

"Harmonize hakufunga ndoa Jumamosi iliyopita, ila alimshirikisha mpenziwe kwenye video ya wimbo wake atakaoutoa hivi karibuni wa 'Marry Me'. Wazo nzima la wimbo huo ni sawia na lile Diamond alitumia na kumshirikisha Zari katika wimbo wake wa 'Iyena'," Mjerumani aliliambia Nyakati.com
 Itakumbukwa kwamba Aprili 2, 2019 Harmonize ambaye jina lake rasmi ni Rajab Abdul Kahali alimposa barafu wa moyo wake Sarah mwenye asili ya Kiitaliano nchini kwao Italy.

Harmonize mwenye umri wa miaka 25 alianza uhusiano wa kimapenzi na Sarah 2017, muda mfupi baada ya staa huyo kutengana na mchumba wake Jacqueline Wolper. 
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad