Mtibwa Sugar yaapa kuifunga Simba


Uongozi wa timu ya  Mtibwa Sugar umesema kuwa kubadilishwa kwa ratiba ya mchezo wao dhidi ya Simba uliopangwa kuchezwa Septemba 18 na kurudishwa nyuma mpaka Septemba 13 uwanja wa Uhuru sio kikwazo kwao katika harakati zao za kupata ushindi.

Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zuber Katwila amesema kuwa hakuna kitakachowazuia wao kufanya vyema kwenye mchezo wao wa pili wa ligi kuu soka Tanzania bara dhidi ya Simba.

Neymar kupigwa bei Januari 2020
“Timu ikiwa imejiaandaa kutafuta matokeo hakuna kinachoweza kuzuia kupata ushindi, sasa kwa kuwa ratiba imebadilika kwetu sio tatizo tutawafuata Simba kwa tahadhari tukizitafuta pointi tatu hata ingekuwa leo hakuna kinachoshindikana,” amesema Katwila.

Kagere, Mayanga waibuka vinara mwezi Agosti
Mtibwa inawasili Dar es Salaam kesho kwa ajili ya kuivaa Simba ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wake wa kwanza mbele ya Lipuli kwa kufungwa mabao 3-1 na Lipuli FC.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA APP YA UDAKU SPECIAL BONYEZA HAPA  

Loading...

Mtibwa Sugar yaapa kuifunga Simba Mtibwa Sugar yaapa kuifunga Simba Reviewed by Udaku Special on September 12, 2019 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.