Askari 6 Akiwemo wa JWTZ Wakuhumiwa kwa Wizi wa Mafuta ya Ndege

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu askari sita akiwemo Mwanajeshi wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) kulipa faini ya Sh 500,000 kila mmoja bada ya kukiri shtaka la wizi wa mafuta ya ndege (Jet A-1/Ik).



Askari hao ni Koplo Shwahiba(38), MT. 74164 SGT Ally Chibwana (47) wa JWTZ, PC Elidaima Paranjo (38), PC Simon (28), PC Dickson na PC Hamza Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi, Vick Mwaikambo baada ya Washtakiwa hao kukiri shtaka linalowakabili.



Mwaikambo alisema kwa kuwa Washtakiwa hao ni kosa lao la kwanza hivyo mahakama hiyo imewapa adhabu ya kulipa faini hiyo kila mmoja na madumu 109 yenye mafuta hayo yatarudishwa serikalini.



Awali wakili wa Serikali Mwandamizi Renatus alidai kuwa awali wastakiwa hao walikuwa wanakabiliwa na makosa matatu hivyo walikubaliana kuliondoa shtaka la kwanza la kupanga genge la uhalifu na shtaka la tatu ni la utakatishaji wa fedha na shtaka la pili la wizi limebaki.



Washtakiwa hao wanadaiwa kuwa Julai 30, mwaka huu katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere uliopo jijini Dar es Salaam, waliiba lita 2180 za mafuta ya ndege (Jet A-1/Ik) yenye thamani ya Sh 4,647,760 mali ya ATCL.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad