10/12/2019

Baada ya hukumu kufutwa Sugu aeleza kinachofuata

 
Mbunge wa Mbeya Mjini kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu, amesema kuwa atakaa na mawakili wake ili kujua nini cha kufanya kwa lengo la kuhakikisha hakuna mwananchi mwingine anafungwa kiholela kama alivyokuwa amefungwa yeye.

Akizungumza na EATV&EA Radio Digital, Sugu amesema kuwa licha ya kuishukuru Mahakama kwa kuamua kutenda haki dhidi yake, iko haja ya yeye kuhakikisha anaisimamia haki ya watanzania wengine wanyonge wanaokumbana na hali hiyo.

''Hukumu hii ni faida kwa Demokrasia na masuala ya Utawala Bora, nitakaa na Mawakili wangu kwasababu hili suala sio 'personal', nilivyofungwa mimi athari yake haikuwa kwangu, kwahiyo tutakaa ili kuangalia ni hatua gani inafuata kwa nia ya kuzuia hiki kitu kisitokee kwa mtu mwingine, tena mimi ni Mbunge na nina 'Status' yangu kama naweza nikafungwa kihuni na kiholela, vipi maelfu ya watu walioko huko magerezani''amesema Mbunge Sugu.

Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya jana Oktoba 11, 2019, ilimfutia hukumu yake iliyokuwa imemfunga gerezani kwa muda wa miezi sita, ambapo alitumikia mitano pamoja na Katibu wa chama hicho, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga kwa kile kilichoelezwa kuwa hukumu hiyo ilikuwa ni batili.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger