Hapo kale: Mambo sita Ya Malkia Elizabeth ii Usiyo yajua

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Malkia Elizabeth II ndiye mtawala katika koo ya kifalme aliyetawala kwa muda mrefu zaidi Barani Uingereza, ambaye alipokea kijiti cha uongozi kutoka kwa babayake Mfalme George vi, mwaka 1952.

Alizaliwa April 21, 1926, hadi sasa ni wapili kwa viongozi walio na umri mkubwa zaidi duniani ambao bado wapo madarakani.

Malkia Elizabeth II amekuwa akiigizwa katika filamu mbalimbali, moja ya filamu maarufu ni The Crown, ambayo Olivia Colman amevaa uhusika wa malkia, swali zuri la kujiuliza ni kwakiasi gani unamfaham Malkia huyu?, hizi ndio sifa sita za malkia ambazo watuwengi bado hawajazifahamu au wamesha zisahau.

i) Hakutarajiwa kuwa Malkia

Licha ya kuwa na desturi kwamba kila mtoto anayezaliwa katika familia ya kifalme ana nafasi yakuwa kiongozi yani kuwa malkia au Mflme, kuna utaratibu wakurithishana ambao hufuatwa na baadhi ya watoto katika mafilia tofauti za ufalme mmoja hujua kabisa kama nafasi haziwezi kuwadondokea.

Ndivyo ilivyokuwa kwa Elizabeth ii, kwani uongozi ulitakiwa kuwa kwa familia ya mjomba wake Edward wa vii , lakini alijiengua katika mnyororo baada ya kumuoa mwanamke aliye achwa na mumewe jambo ambalo ni kosa kwenye fmilia yao kuoa mwanamke aliyeachika.

Hivyo baba yake Malkia Elizabeth ii, Georgre vi, ndiye aliyepewa kijiti cha kuwa mfalme na kuwasha taa kwenye njia ya Elizabeth kuwa malkia, ambaye alirithi kijiti baada ya kifochake.

ii) Ni mke na Mama wa watoto wa nne

Malkia Elizabeth ii, aliolewa novemba 1947 baada ya kutimiza mika 21, na Binamu yake Prince Philip ambaye wameshea bibi mzaa bibi yaani wote ni vilembwe wa Malkia Victoria.

Walifanikiwa kupata watoto wanne ambao ni Prince Charles, Princess Anne, waliozaliwa kabla Elizabeth hajawa malkia, Prince Andrew na Prince Edward walizaliwa baada ya kuwa Malkia.

Elizabeth ii na mwanae Prince Charles kabla hajawa Malkia mwaka (1952)

iii) Anauchukia mwaka 1992

Kama ilivyo kwa watu wengine ambao hujikuta kwasababu tofauti wanazichukia siku, tarehe, au mwaka, basi Malkia naye anamwaka anaouchukia sana ambao ni 1992.

Mwaka huu haukua mzuri kwake na kwafamilia yake kwani kwasababu tofati Ndoa za watoto wake watatu zilivunjika, Prince Charles, Prince Andrew na Princess Anne.hivyo aliamua kuuita mwaka mbaya zaidi kwao.

iv) Amewahi kupokea zawadi za kustaajabisha

Malkia elizabeth amewahi kupewa zawadi za kustaajabisha wakiwemo wanyama, kama ilivyo desturi kwa baadhi ya watu kupewa wanyama  waendapo kusalimia nduguzao kama Babu, Bibi, wajomba na Shangazi.

Malkia alipewa kobe wawili mwaka 1972 alipokuwa anatalii Seychelles, pia alipewa mtoto wa Tembo aliyeitwa Jumbe, na Rais wa Cameroon mwaka huo huo 1972.

v) Ameshuhudia Marais 13 wa USA wakiingia madarakani tokea awe Malkia

Tangu ashike rasmi umalkia wa Uingereza , Elizabeth ameongoza sambamba na Marais 13 wa Marekani ambao ni Rais Harry Truman aliyemkuta madarakani mwaka 1947, Dwight Eistenhower 1953, John F. Kenedy 1961, Lyndon Johnson 1963, Richard Nixon 1969, Gerald Forld 1974, Jimmy Carter 1977, Ronald Reagan 1981, George H W Bush 1989, Bill Clinton 1993, George W Bush 2001, Barack Obama 2009, na Donald Trump 2017, bado yupo madarakani na malkia bado hajaachia kijiti ambacho anaweza kupokea mwanae Prince Charles au atarithi akifariki.

vi) Nikosa kuendelea kula Malkia akishiba

Kuna mengi sana ya kustaajamisha yanayomhusu Malkia Elizabeth ii, leo tumalizie na hili, Endapo mtu yeyote akapata bahati yakula na Malkia meza moja basi sheria kuu ya kuzingatia ni kwamba malkia akisha shiba na kuweka kijiko mezani , watu wote mnatakiwa kuacha kula kwani nikosa kuendelea kula baada yake.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad