10/07/2019

Jaji Ajipiga Risasi Katika Chumba cha Mahakama


JAJI Kanakorn Pianchana wa Thailand amejipiga risasi kifuani katika chumba cha mahakama baada ya kuwaachia huru watuhumiwa watano wa mauaji. Alitaka kujiua alipomaliza hotuba yake akishinikiza uwepo wa mfumo huru na wazi wa kimahakama kumtia mtu hatiani. Sasa anapatiwa matibabu.Wachambuzi wa mambo wanasema mahakama za Thailand kila mara kuwapendelea matajiri na wenye madaraka, lakini huwa zinatoa hukumu za haraka na ngumu kwa watu wa kawaida kwa makosa madogo jambo ambalo majaji huwa hawalilalamikii.Jaji huyo alikuwa ameaachia Waislam watano waliokuwa wakituhumiwa kwa kuua kutumia bunduki Ijumaa iliyopita ambapo baada ya kufanya hivyo alitoa bastola na kujipinga kifuani.“Unatakiwa kuwa na ushahidi wa wazi na wenye kuaminika ili kumwadhibu mtu.  Hivyo, kama huna uhakika, usimwadhibu,” alisema jaji huyo kortini hapo.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger