10/12/2019

JPM Azindua Safari zya Ndege Kutoka Dar Kwenda Mpanda


Rais John Magufuli  leo Jumamosi Oktoba 12, 2019 amezindua safari za Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kutoka Dar kwenda Mpanda mkoani Katavi.

Amesema hadi leo Jumamosi watu 138 waliokuwa wakidaiwa kuwa na mashtaka ya uhujumu uchumi na kuomba msamaha kwa DPP, wamerudisha fedha, wametubu na kuachiwa.

Aidha,ameongeza kwamba:

“Walioachiwa wako huru wamekwenda kujumuika na familia zao. Huo ndiyo upendo wa pekee kwa sababu tulitoa msamaha na wao wamepokea na sisi tunashukuru. Hao sasa ni raia wema wahesabike kuwa ni raia wema katika nchi yetu.”

Amesema kulikuwa na watuhumiwa 700 walioomba msamaha na wataendelea kuachiwa kadri watakavyorudisha fedha na fedha hizo zitatumika katika shughuli za maendeleo

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger