10/05/2019

Magufuli Amnyooshea Kidole Mwele Malecela Asema Alitumiwa na Mabeberu Kutangaza Ugonjwa 'Hewa' wa ZikaAkielezea ni kwa namna gani humpelekea kufanya kazi hadi usiku Rais Magufuli amesema katika vita hasa ya kiuchumi adui mbaya zaidi hutoka ndani kwa maana ndiye huwa kiungo wa maadui wa nje.

Ametolea mfano wa aliyekuwa Mkurugenzi wa NIMR TANZANIA Bi Mwele Malecela alilazimika kumfuta kazi baada ya yeye kutoa taarifa za uongo kwamba wakati ule kulikuwa na ugonjwa wa Zika ilhali haikuwa kweli.'Je huo ugonjwa wa Zika ulionekana tena!?'alihoji Mheshimiwa Rais!

Amesema hali hiyo ya Mwele kuutangazia uongo Ulimwengu kuhusu uwepo wa zika Nchini Tanzania ilimkwaza sana na dhahili alionekana kutumiwa na washindani wa vita ya kiuchumi na Nchi yetu.

'Na ndiyo maana baada ya kumfuta kazi wiki moja baadae waliomtumia walimpa kibarua kingine'alisema Mheshimiwa Rais.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger